You are here: Home

Chombo Chetu Edition 44

PreviewChombo Chetu is a Diocesan magazine published thrice a year. Edition 44 is the latest edition and it is out!! Just to give you an overview...

Ujanja na ujuaji haufai katika huduma,

Ujanja na ujuaji haufai katika hudumaMchungaji analiwa matendo yake Wachungaji wanahimizwa kujiepusha na ujana na ujuaji wanapofanya kazi ya Mungu. Askofu Mstaafu Jeremiah Taama aliyasema haya alipokuwa akihubiri wakati wa ibada maalum ya kupeana daraja mbali mbali wahudumu wa kanisa Anglikana Dayosis ya Taita Taveta Disemba 13, 2015 Voi. Askofu alisema kuvunjika na kutubu dhambi ni jambo muhimu katika maisha ya mhudumu. Akizingatia maandiko kutoka kwa Marko 14: 22, Askofu alisema kama vile Yesu Kristo aliumega na kuuvunja mkate, wakristo wanapaswa kuwa watu wa kukubali kuvunjika na kutubu dhambi ili kumruhusu roho wa Mungu kuwa ndani yao. Askofu alisema wahumu wanapaswa kuwa mfano mzuri wa kuigwa na wakristo wanapohubiri na kwafundisha na kuwaelekeza kwa Mungu. Aliendelea kusema kuwa matendo yake Mhudumu yanaliwa na watu wote. “Uwe mfano mzuri na wacha watu wakutamani”. alisisitiza Askofu. Askofu Taama alisema siri ya kutuoa hudumu nzuri na ya kubariki ni Yesu Kristo kuwa kuwa ndani ya moyo na Yesu Kristo kuwa ndani. Alitoa wito kwa wahudumu kujipeana kwa mikono ya Mungu ili waweze kufanywa vyombo vya kufanya huduma iliyo ya kiwango cha juu. .......

 


 

Uwezo wa mkono wa Mungu?

Uwezo wa mkono wa Mungu Mtoto anapozaliwa matumaini yake makubwa ni kwa mzazi wake. Kila motto anapokuja duniani huja na kipawa fulani ambacho Mungu hutazamia kitatukuzwa kupanua kazi yake. Uwezo wa mkono wa Mungu huwa juu ya kila mwanadamu lakini jamii na dunia nzima hufanya yanayowezekana yawe hayawezekani. Basi hapo mtoto anapokua hujifunza mengi yasiyowezekana na kufungia nje yanayowezekana . Mfano mzuri ni Mariamu alipojiwa na Malaika aliamini haiwezekani yeye kuwa mzazi wa mkombozi wa dunia . Lakini sauti ya Mungu ilimuhimiza kuwa yote yawezekana. Tunapaswa kuwafunza watoto na Jamii nzima juu ya uwezekano wa kufaulu kuliko changamoto zinazotuzuia kufikia malengo yetu. Inawezekana mwaka wa 2016 tukawa na ufanisi mkubwa zaidi kuliko miaka yote kama tutakubali kuishi kwa jangwa la kujitolea(Desert of commitment) kuliko kuwa kwa kasri (palace)ya kutukuzwa. .

.

Pili......... 

 


 

Wizi wa madawa wakemewa

Viongozi wa Kaunti ya Taita Taveta wameeleza masikitiko yao juu wizi wa madawa katika hosipitali za uma.

Wakiongea katika katika mkutano ambao uliandaliwa Voi Machi 12,2014,  viongozi waliomba serikali ya kaunti iingilie kati na kufanya uchunguzi ili wanaojihusisha na vitendo hivyo wachukuliwe hatua kali.

Akizungumza katika mkutano huo wa kusambaza madawa kwa hospitali za uma  , Gavana John Mruttu  alitoa onyo kali kwa maafisa watakaopatikana wakiuza madawa yanayokusudiwa kusaidia wananchi.

Gavana alisema......

 


 

To read more please purchase your copy of the Chombo Chetu @Ksh 50 at any parish or visit the Diocesan office in Voi (Ekklesia House)

Find us on Facebook

Tweet us (2)

ackttvt We thank God for a successful ACK Taita Taveta Diocesan Mother's Union Charity Walk 2018.
ackttvt Anglican Church of Taita Taveta moves digital...
Chalasah Designed It.