You are here: Home

Chombo Chetu 52

Chombo 52 edited

Chombo Chetu is a Diocesan publication published quaterly to diseminate information of activities taking place in the Diocese.Edition number 52 is out .Get your copy from our ACK Churches in Taita Taveta County.

Je ni lazima uwe mshirikina kuchimb madini

Madini ni raslimali muhimu kutoka kwa Mungu  hivyo basi hayapaswi kamwe kushikanishwa na mambo ya ushirikina. Wakristo wengi wamekuwa hawajishuhulishi na kazi ya kuchimba madini kwa sababu yameshikanishwa na  ushirikina.  Wakizungumza katika warsha iliyoandaliwa Voi na shirika la Maendeleo Angilican Development  Services Pwani  mapema mwaka huu kuhusu  madini viongozi  walisema  dhana kuwa madini yanashikanishwa na uchawi ni ya uongo na inalenga kuzuia wakristo kuchimba na kuuza madini. Kaunti ya Taita Taveta ni moja ya Kaunty iliyo na madini mengi nchini Kenya. Jambo la kushangaza ni kwamba Kaunti ya Taita Taveta  ni moja ya zile Kaunti ambazo zinakumbwa na umaskini wa kiwango cha juu. Uchimbaji madini haujafaidi jamii ya wataita na wataveta kwa sababu hakuna sera  za kuendesha biashara ya uchimbaji na uuzaji wa madini. Mashirika ya kijamii yamekuwa yakipigania haki katika uchimbaji wa madini  yakidai kuwa  kumekuwa na unyanyasaji na ukosefu wa usalama kwa wafanyi kazi miongoni mwa matatizo mengine..

Katika warsha hiyo, waakilishi wa Kanisa na mashirika ya kijamii walihamasishwa kuhusu sheria  ya madini na kuhimizwa kuzingatia   sekta ya uchimbaji madini kama njia moja ya kujikwamua kutoka kwa umasikini.

Akizungumza katika warsha hiyo, Askofu Liverson Mng’onda  alisema ni sharti watu washikane na Mungu kama wanataka kufanya mambo tofauti. Askofu aliongeza kusema  mara nyingi  ni watu wachache hujitolea kutetea haki ya wanyonge . Askofu aliwahimiza washiriki  kufanya mambo tofauti ambayo yatachangia kuleta mabadiliko kwa maisha  ya wananchi.

Naye  mtalamu  wa Kaunti  katika mambo ya madini Bwana Edward Omito  akizungumza alisema kuna madini mengi katika Kaunti  ya Taita Taveta lakini kazi ya uchimbaji madini  inafanyika kwa kiwango cha chini sana ikilinganishwa na nchi jirani  kama vile Tanzania. Bw. Omito alitoa wito kwa wanaochimba madini kufuata sheria kwa kukata leseni na kufanya biashara yao kupitia kwa ofisi yake ili kuzuia kudhulumiwa. Omito alihimiza kanisa kuwa mstari wa mbele kuelimisha wananchi kuhusu sheria ya madini nchini ili kupunguza dhuluma na ukiukaji wa haki katika sekta ya madini.

Find us on Facebook

Tweet us (2)

ackttvt We thank God for a successful ACK Taita Taveta Diocesan Mother's Union Charity Walk 2018.
ackttvt Anglican Church of Taita Taveta moves digital...
Chalasah Designed It.