You are here: Home

Chombo Chetu Edtion 53

 
Edited for web
Bishop Liverson consecrated and launched the latest issue of our Diocesan News letter Chombo chetu.The Newsletter will be distributed to all Parishes. Get your Copy  to get  latest diocesan news.
 
Ndoa zimekuwa uwanja wa fujo
Ndoa ni  makubaliano ya mwanamke na mwanamme kuishi pamoja kama mke na mme. Watu wanapoingia katika ndoa huwa na matumaini makubwa ya kuishi kwa furaha  na amani. Ndoa nyingi zinayumbayumba na hata zingine zinavunjika kila kuchao. Akizindua kitabu ‘Marriage bila Regets‘ kilichoandikwa na Mchungaji Mark Kithokilo,Askofu Liverson Mng’onda alieleza masikitiko juu ya  vita vya mara kwa mara kati ya waliooana  akisema ndoa zimekuwa uwanja wa fujo. Askofu  alisema kila mara visa vya watu walio katika ndoa kujeruhiana na hata kuana  vinaripotiwa jambo ambalo ni la kuhuzunisha sana.  Askofu alimpongeza Mchungaji Mark kwa kuandika mambo ya ndoa akieleza juu ya kuepukana na  majuto katika ndoa. Alihimiza watu kukisoma kitabu hichoambacho kinalenga vijana ili kuzuia mafarakano ndani ya ndoa. Akiongea wakati wa uzinduzi Mchungaji Mark alisema ameandika  vitabu juu ya ndoa akiwa na matumaini ya kufundisha watu vile wanaweza kuingia kwa ndoa  na  kuziimarisha . Wakati huo huo Askofu aliombea na kukibariki kitabu kilichoandikwa na Rajab Mvumba  kinachoitwa “Prerequisite for Success”. Akijibu swali ni nini kilimsukuma kuandika kitabu hiki, Rajab alisema maisha yake yalikumbwa na changamoto nyingi kutokana na hali ya umasikini. Hivyo basi katika kitabu chake anaeleza vile unaweza kufaulu katika maisha licha ya changamoto unazopitia. Kitabu hiki anasema kina manufaa makubwa kwa mwanafunzi , mzazi  na hata mwanabiashara.
 

Find us on Facebook

Tweet us (2)

ackttvt We thank God for a successful ACK Taita Taveta Diocesan Mother's Union Charity Walk 2018.
ackttvt Anglican Church of Taita Taveta moves digital...
Chalasah Designed It.