You are here: Home

Chombo Chetu 54th edition

December 2018 January 2019 262

Bishop Liverson consecrated and launched the latest issue of our Diocesan News letter Chombo chetu.The Newsletter will be distributed to all Parishes. Get your Copy  to get  latest diocesan news

Lazima kanisa   liheshimiwe

Ni lazima heshima ya kanisa idumishwe kila wakati  na kila mkristo. “Si  tabia nzuri kwa muanglikana kusoma neno la Mungu kutoka kwa simu ya mkononi  akiwa kanisanai  badala ya kubeba Bibilia”. Askofu Charles Muturi wa Dayosis ya Mt. Kenya South alisema haya alipokuwa  akihubiri kwa ibada maalum ya kuwapa daraja wahudumu  Disemba 8,2018. Askofu alisema Kanisa ni mahali patakatifu na ni lazima liheshimiwe . Askofu alieleza masikitiko yake juu kuzorota  kwa maadili mema ya kudumisha  heshima kwa kanisa  na viongozi akisema tabia hiyo lazima ikome.  Wachungaji hawapaswi kwenda  kumuona Askofu bila  kuvaa  nguo za kazi na kola . Si heshma   kwa waumini  au wahudumu kuendelea kufanya mawasiliano kwa simu wakati wa ibada au wakati wowote neno la Mungu linahubiriwa. “Siwezi kuchukuwa simu nikiwa kwa ofisi ya Askofu mkuu”  alisema Askofu Muturi. Askofu  aliwahimiza wahudumu kumuheshimu Askofu na ngazi zote za uongozi wa kanisa ili kudumisha heshima ya Kanisa Anglikana. Hali kadhalika Askofu alitoa wito kwa kila mmoja kuwa na nidhamu ya hali ya juu anapofanya huduma  ya Mungu.

Waliopewa daraja ya kuwa kasisi katika ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Liverson Mng’onda ni Jemimah  Mwarong’e, Tumaini Lukwaro Jumanne,Brian Makeo ,Benson Nyoro na Isaac Mwambingu. Waliofanywa kuwa mashemasi ni  Priscillah Mwakiaro, Charles Ponga na Harison Mwabili. Waliopewa daraja ya kuwa wainjilist ni Julius Konde,Anthony Mghanga na Erick Mwasho.

Mchungaji Geofrey Lamisi alipewa daraja mpya ya kuwa Archdeacon. Mchungaji Benard Kilonzo  na mwenzake Duncan Kibula walifanywa kuwa Rural deans.

Find us on Facebook

Tweet us (2)

ackttvt We thank God for a successful ACK Taita Taveta Diocesan Mother's Union Charity Walk 2018.
ackttvt Anglican Church of Taita Taveta moves digital...
Chalasah Designed It.